Tuesday, 15 November 2011

Hymn- Kiswahili

KAA NAMI NI USIKU SANA
Usiniache gizani Bwana
Msaada wako haukomi
Nili peke yangu kaa nami

Siku zetu hazikawi kwisha
Sioni la kunifurahisha
Hakuna ambacho hakikomi
Usiye na mwisho kaa nami

Nina haja nawe kila saa
Sina mwingine wa kunifaa
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe Bwana kaa nami

Sichi neno uwapo karibu
Nipatalo lote si taabu
Kifo na kaburi haviumi
Nitashinda kwako kaa nami

Nilalapo nikuone wewe
Gizani mote nimulikie
Nuru za mbinguni hazikomi
Siku zangu zote kaa nami.

No comments:

Post a Comment