NI TABIBU WA KARIBU
Tabibu wa ajabu
Na rehema za daima
Ni dawa yake njema
Imbeni malaika
Sifa za Yesu Bwana
Pweke limetukuka
Jina lake Yesu
Hatufai kuwa hai
Wala hatutumai
Ila Yeye kweli ndiye
Atupumzishaye
Dhambi pia na hatia
Ametuchukulia
Twenendeni na amani
Hata kwake mbinguni
Huliona tamu jina
La Yesu Kristo Bwana
Yuna sifa mwenye kufa
Asishindwe na kufa
Kila mume asimame
Sifa zake zivume
Wanawake na washike
Kusifu Jina Lake
Na vijana wote tena
Wampendao sana
Waje kwake wawe wake
Kwa utumishi wake.
No comments:
Post a Comment