TUFANI INAPOVUMA
Sana moyoni mwangu
Huona pa kujificha
Mkononi mwa Mungu
Hunificha hunificha
Adui hatanipata
Hunificha hunificha
Mkononi Mwake
Pengine kuna taabu
Yanisongeza kwake
Naijua si hasira
Ni ya mapenzi yake
Adui wakiniudhi
Nami nikisumbuka
Mungu atavigeuza
Vyote viwe baraka
Niishipo duniani
Ni tufani daima
Anilindapo rohoni
Nitakaa salama.
No comments:
Post a Comment